CHAN (African Nations Championship) ni mashindano ya kila baada ya miaka minne yaliyoanzishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya timu za Taifa za Afrika. Lengo la mashindano haya ni kutoa fursa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani za nchi zao kushiriki katika michuano ya kimataifa.
Michuano ya CHAN 2024 itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania. Hapo awali mashindano hayo yalikusudiwa kufanyika Februari 1-28, lakini yaliahirishwa kwa lengo la kutoa muda zaidi kwa nchi waandaaji kufanya maandalizi.
Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la Mwananchi, maandalizi hayahusu viwanja pekee, kama ambavyo watu wanadhani, kuna viwanja vya mazoezi, usafiri wa mashabiki, hoteli, hospitali na mambo mengine mengi yanayohitajika kwa mashindano ya aina hii.
Mashindano ya CHAN 2024 hatimaye yatafanyika Agosti 2 hadi 30 2025. Ni kwa mara ya kwanza CHAN kuaandaliwa na nchi tatu za Afrika mashariki, hiyo hi historia mpya itakuwa imeandikwa, lakini historia hiyo itakuwa bora zaidi ikiwa moja ya timu wenyeweji itahakikisha kombe linabaki katika jumuiya hii.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni