Breaking


Alhamisi, 20 Novemba 2025

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA, imetoa utabiri wa saa 24 zijazo na kueleza kuwa mvua na ngurumo zinatarajiwa katika mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe, huku mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Morogoro, Ruvuma, Lindi na Mtwara ikitarajiwa kuwa na mvua katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua. Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na mawingu kiasi na mvua nyepesi katika baadhi ya maeneo.



TMA imetoa tahadhari ya uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika maeneo machache ya Songwe, Mbeya, Njombe, Rukwa, Iringa, Ruvuma, Morogoro, Singida na Dodoma, na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari. Aidha, upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kaskazini mashariki kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa, na bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.



Kwa mujibu wa TMA, viwango vya joto vya juu vinatarajiwa kufikia nyuzi 33 Dar es Salaam na Dodoma, nyuzi 30 Mwanza, nyuzi 29 Kigoma na Arusha, huku Zanzibar ikitarajiwa kufikia nyuzi 31. TMA imesema matarajio ya Jumamosi, Novemba 22, ni mabadiliko madogo ya hali ya hewa.


Hakuna maoni: