SEHEMU YA KWANZA: (1)
Kijijini Mbuyuni, kilicho ndani ya bonde lenye vumbi lenye miti midogo na nyumba za udongo zilizopakwa mchanga, aliishi Neema, binti mdogo mwenye macho makubwa yaliyojaa hofu na ndoto. Alizaliwa kwenye familia iliyokumbwa na huzuni: baba yake alifariki akiwa mdogo kutokana na ugonjwa, na mama mzazi alifariki muda mfupi baadaye.
Neema alibaki chini ya ulezi mkali wa mama wa kambo, mwanamke mkali asiye na huruma, aliyemfanya Neema ajihisi mzigo wa kila siku. Kila asubuhi kabla jua kuangaza, Neema alikua akifanya kazi zisizoisha: kuchota maji kutoka kisima kilichoko umbali wa kilomita kadhaa, kulima shamba dogo la mahindi, kuchunga mbuzi na kuku, na kuosha vyombo vyote vya familia.
Hali ya mavazi yake ilikuwa ya kusikitisha: nguo zilizochanika, zikiwa zimejaa vumbi na machungu ya miaka ya mateso, zinazoonyesha historia ya kila kipigo cha maneno na dhihaka aliyopitia.
Ndani ya moyo wake mdogo, Neema alikuwa na ndoto kubwa: kuondoka kijijini, kuona dunia kubwa na kuishi maisha ya heshima, mbali na dhuluma ya mama wa kambo. Hata kama alikosa nguvu na rasilimali, ndoto hiyo ilikuwa msingi wa kuishi kwake. Kila jioni, alipokuwa chini ya mti wa miembe akitazama barabara kuu, alijiuliza: Je, siku moja maisha yangu yatawahi kubadilika?
Aliishia kutabasamu na kuandika kwenye ukuta maneno yasiyoeleweka maana hakujua kusoma wala kuandika sababu hakuwahi kupelekwa shule, alichokiandika na kukielewa yeye mwenyewe ni haya maandishi… YHTKAHQU (akimaanisha siku itafika) 😃😃😃 unabisha ulikuwepo😃😃

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni