Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeipongeza Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya michezo kuelekea Michuano ya AFCON 2027.
Kamati hiyo imetoa pongezi hizo leo, Februari 12, 2026 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, wakati wakipokea taarifa kuhusu mchango wa Sekta ya Habari katika kufikia malengo ya Dira ya 2050 pamoja na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya mashindano ya Mashindano ya AFCON 2027.
Katika michango ya Wajumbe kamati hiyo, wameitaka Wizara kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika maandalizi ya mashindano hayo ili ilete matokeo chanya kwenye jamii.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni