Breaking


Jumatatu, 30 Machi 2026

FITCH YAITHIBITISHIA TANZANIA DARAJA LA ‘B+’, MTAZAMO WAENDELEA KUWA THABITI

Kampuni ya tathmini ya nchi kukopa na kulipa mikopo ya Fitch Ratings, imeithibitisha Tanzania kuendelea kuwa ‘B+’ huku likidumisha mtazamo wa “Stable Outlook”. Hatua hiyo inaashiria imani ya Kampuni hiyo katika mwenendo wa uchumi wa nchi pamoja na uthabiti wake wa kifedha katika kipindi cha kati.


Kwa mujibu wa tathmini hiyo, Tanzania inaendelea kunufaika na ukuaji mzuri wa pato la taifa (GDP) , kiwango cha chini cha mfumuko wa bei, deni kuendelea kuwa himilivu ikilinganishwa na nchi nyingine zinazofanana.


Mwenendo mzuri wa uchumi umepelekea upatikanaji wa fedha za nje kupitia programu za Shirika la Fedha la Kimataifa - IMF ikiwemo Extended Credit Facility (ECF) inayohusisha upatikanaji wa mkopo nafuu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta za uzalishaji na huduma za jamii na Resilience Sustainability Facility (RSF) ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Ripoti hiyo pia imeeleza kuwa ushindi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi

Hakuna maoni: