Breaking

Alhamisi, 14 Agosti 2025

DKT. MAPANA: BASATA KUENDELEA KUSIMAMIA UBUNIFU, MAADILI NA UBORA WA KAZI ZA SANAA KUKUZA UCHUMI WA TAIFA

 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana, amewasilisha hotuba yenye msukumo mkubwa kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na BASATA, katika Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2025 na Mashariki Creative Economy Expo 2025 linalofanyika Mlimani City kuanzia leo tarehe 14 hadi 16 Agosti 2025.

Katika hotuba yake, Dkt. Mapana alieleza kwa kina majukumu ya BASATA, ikiwemo usajili wa wasanii na kazi za sanaa, utoaji wa leseni za shughuli za sanaa, uratibu wa matamasha, na utoaji wa mafunzo kwa wasanii ili kuongeza ubora na ushindani wa kazi zao sokoni, kusimamia maadili ya kazi za sanaa, na kuhamasisha ubunifu unaochangia ukuaji wa uchumi wa taifa, aidha Dkt. Mapana aligusia juu ya maendeleo ya teknolojia ya uunganishaji wa mifumo mbalimbali inayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kama vile BRELA, NIDA,TRA na mifumo mingine

Dkt. Mapana aliwahimiza wadau wa sanaa kutumia fursa zilizopo kwenye tamasha hili kujifunza, kujenga mitandao ya kibiashara na kuendeleza kazi zao kwa kufuata miongozo na sheria za sekta ya sanaa. Alibainisha kuwa BASATA itaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha tasnia ya sanaa inakuwa endelevu na yenye mchango mkubwa kwa pato la taifa.





Hakuna maoni: