RASMI: Vilabu vya watani wa Jadi vya Simba Sc na Yanga Sc wote wamewatambulisha walinzi wao wazawa wa kushoto kwaajili ya msimu mpya wa mashindano 2025/2026.
Klabu ya Simba kupitia taarifa yao ilithibitisha kukamilisha usajili wa Anthony Mligo mwenye umri wa miaka 17 kwa mkataba miaka mitatu (3) kutokea klabu ya Namungo Fc wakati Yanga Sc ikimtambulisha Mohamed Hussein Tshabalala maarufu kama 'Zimbwe Jr' mwenye umri wa miaka 28 kutokea kwa majirani zao hao hao Simba Sc kwa mkataba wa miaka miwili (2) baada ya mchezaji huyo kudumu Simba Sc kwa miaka 11 toka aliposajiliwa Kagera Sugar akiwa na miaka 18 mwaka 2014.
NB: Usajili na Anthony Mligo kwa wekundu wa msimbazi Simba sc unakuwa usajili wa saba (7) klabuni hapo baada ya usajili wa beki Rushine De Reuck, Kiungo Alassane Maodo Kante, Winga Morice Abraham, Kiungo Mkabaji Hussein Daudi Semfuko kutokea klabu ya Coastal Union, Jonathan Sowah kutokea Singida Black Stars na Mohamed Bajaber kutokea Kenya Polisi ya nchini Kenya.
Wakati kwa upande wa Yanga Sc usajili wa Mohamed Hussein Tshabalala unakuwa usajili wa tisa (9) mpaka sasa kwenye utambulisho wa kikosi cha chao baada ya usajili wa Kiungo mshambuliaji Mohamed Doumbia, Kiungo Celestin Ecua, beki Abubakar Nizar Othuman (Ninja), Kiungo Moussa Balla Conte, Winga Offen Chikola, Kiungo Abdulnasir Mohamed na kocha Romain Folz ambao wametambulishwa mpaka sasa kunako viunga vya Jangwani.
#Anoldmathias255✍🏾
#TukutaneUwanjani⚽️




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni