Manchester United haitaendelea na mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Cameroon Carlos Baleba, 21, msimu huu wa joto, huku thamani ya Brighton ya pauni milioni 115 ikionekana kuwa juu sana. (Athletic - subscription required)Kipa wa Manchester City Ederson, 31, anafikiria mustakabali wake katika klabu hiyo na uwezekano wa kwenda Galatasaray. Iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ataondoka, City itataka kumsajili mchezaji wa Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma, 26, huku nyota huyo wa Italia akipatikana. (Guardian)
#ChanzoBbcswahili


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni