Ecobank Tanzania imezindua kampeni maalum ya “Gutuka na Ecobank” ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya huduma zake barani Afrika na miaka 15 tangu kuanza kwa huduma zake hapa nchini Tanzania.
Uzinduzi wa kampeni hiyo na utadumu kwa miezi mitatu, ambapo wateja watakaoweka akiba kupitia akaunti ya Supa Seva watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki za miguu mitatu (Gutas) na pesa taslimu hadi shilingi milioni moja.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Innocent Urio amesema kampeni hiyo inalenga kuhamasisha watanzania kuthamini utamaduni wa kuweka akiba.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara Wadogo na Wakati (SME), Juma Hamisi, alisisitiza kuwa wafanyabiasha sasa wana nafasi ya kunufaika na kampeni ya Gutuka na Ecobank ambapo mteja atakayefungua akaunti ya Supa Seva inampa mteja riba hadi asilimia 5 kwa robo mwaka bila makato ya mwezi, fursa ya kutoa pesa bure mara moja kila mwezi na huduma ya Lipa Namba bure kwa wateja wa SME na kadri mteja anavyoweka akiba zaidi, ndivyo anavyozidisha nafasi ya kushinda zawadi kubwa.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni