Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Klabu ya Simba pamoja na mashabiki wake kwa kuandaa tamasha kubwa na lenye kuvutia la Simba Day 2025.
Rais Samia amepigasimu na kuwatakia kila la kheri katika msimu mpya wa mashindano ya kitaifa na kimataifa, huku akiwataka kuendeleza nidhamu, mshikamano na ushindani wa kimataifa ili kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.
“ Ninawapongeza Klabu ya Simba na Wanasimba kwa tamasha zuri la Simba Day 2025. Ninawatakia kila la kheri katika msimu ujao kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa.”
Aidha, Rais amesisitiza kuwa michezo ina nafasi muhimu katika kudumisha mshikamano wa kitaifa, kujenga afya za vijana na kuimarisha umoja wa Watanzania kupitia mashindano ya kitaifa na ushiriki wa klabu katika ngazi za kimataifa.
Kwa upande wao, uongozi wa Simba SC umemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa pongezi na maneno ya hamasa, wakiahidi kuendeleza nidhamu, mshikamo na juhudi za kuhakikisha timu inapata mafanikio makubwa zaidi ndani na nje ya Tanzania.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni