Breaking

Jumatatu, 8 Septemba 2025

SBL NA NCT WAZINDUA AWAMU YA PILI PROGRAMU YA LEARNING FOR LIFE

 

Serikali imewaomba vijana nchini kutumia kikamilifu fursa za ajira zinazotokana na mafunzo ya vitendo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaandaa moja kwa moja kwa soko la ajira, hasa katika sekta ya ukarimu na utalii.

Kauli hiyo imetolewa kufuatia uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya Learning for Life, inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) na Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), katika tawi la NCT jijini Arusha.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa NCT, Dkt. Florian Mtey, amesema programu hiyo ina mchango mkubwa katika kuwaandaa wanafunzi kwa mazingira halisi ya kazi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Christopher Gitau, amesema kampuni hiyo inaamini katika uwekezaji kwa vijana kama njia ya kuimarisha maendeleo ya jamii.

Programu ya Learning for Life ni sehemu ya ajenda ya kijamii ya SBL, ijulikanayo kama Spirit of Progress, ambayo inalenga kuwekeza kwa jamii kwa muda mrefu kwa kuwawezesha vijana wa Kitanzania.

Hakuna maoni: