Breaking

Jumanne, 9 Septemba 2025

TAKRIBANI SHILINGI BILIONI 1.3 YAOKOLEWA GHARAMA ZA KUKODISHA USAFIRI

 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua mpango mpya wa kuboresha huduma kwa wateja kwa kununua vitendea kazi ikiwemo magari 100, bajaji 100 na pikipiki 284, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma bila kujali jiografia ya maeneo wanayoishi wateja wake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba 09, 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, alisema uamuzi huo umefuatia ziara ya Mkurugenzi Mtendaji Bw. Lazaro Twange ambaye alibaini uhitaji mkubwa wa vitendea kazi katika mikoa mbalimbali nchini.

Aidha, hatua hii imepunguza gharama kwa kiasi kikubwa, kwani awali tulikuwa tukitumia shilingi bilioni 1.3 kila mwezi kukodisha magari,” alisema Bi. Gowelle.

Aliongeza kuwa mbali na kurahisisha upatikanaji wa huduma, uwepo wa vitendea kazi hivyo utaboresha pia mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wa TANESCO, ambao ni nguzo muhimu katika kuhakikisha wateja wanapata huduma bora. 

Pia aliwataka watendaji wa shirika hilo kuvihifadhi na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

Vitendea kazi hivyo vinatarajiwa kutumika hususan katika maeneo yenye madawati ya dharura yanayotoa huduma saa 24, ili kuhakikisha changamoto za wateja zinatatuliwa kwa haraka na kwa wakati.

Hakuna maoni: