SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuwa, limeendelea kutenga zaidi ya shilingi milioni 350 kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wenyewe zithibitishwe ubora. wanazozizalisha.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Ashura Katunzi ameyasema hayo leo Septemba 18,2025 katika kikao kazi kati ya wahariri na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Dkt. Katunzi amesema kuwa, wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa wajasiriamali kutokana na mahitaji na wataendelea kuwahudumia kadri inavyowezekana katika halmashauri zote nchini.
Pia, amesema, wataendelea kuwasiliana watendaji katika halmashauri mbalimbali nchini ili kuweza kuwatambua wajasiriamali ambao wana bidhaa zao na wanatamani ziwe katika viwango bora, lakini hawana uwezo ili ziweze kupata soko la ndani na nje.
Vilevile amesema, kupitia maabara 12 za TBS ambazo zimehakikiwa na kupewa vyeti vya ithibati ya Kimataifa zimeendelea kuwasaidia watengenezaji bidhaa kuongeza na kuimarisha ubora wa bidhaa zao.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni