Breaking

Alhamisi, 18 Septemba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI: JUVENTUS YAMTAKA NYOTA WA MAN CITY BERNARDO SILVA

 

Juventus watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva, 31, kwa uhamisho wa bila malipo wakati mkataba wake wa Manchester City utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Tuttosport - In Itali)

Manchester City wanafikiria kumnunua mchezaji wa Manchester United Kobbie Mainoo, ingawa wana uwezekano wa kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Newcastle na Chelsea kumnunua kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 20. (TeamTalks)

Chelsea bado wanavutiwa na Morgan Rogers licha ya kukasirishwa na hesabu ya Aston Villa ya pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 23, msimu wa joto. (The Sun)

#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: