Breaking

Alhamisi, 11 Septemba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI: MAN UTD INAMFUKUZIA ANDERSON NOTTINGHAM FOREST

 

Manchester United inataka kumsajili kiungo wa kati wa Nottingham Forest na England mwezi Januari Elliot Anderson, 22. (Teamtalk)

Arsenal imepiga hatua katika mazungumzo ya kurefusha mikataba ya winga wa Uingereza Bukayo Saka,24, na beki wa Ufaransa William Saliba,24, mikataba hiyo itakapomalizika mwishoni mwa msimu wa 2026-27. (Teamtalk)

Kipa wa Cameroon Andre Onana, ambaye anakaribia kujiunga na Trabzonspor ya Uturuki kwa mkopo, alikataa ofa kutoka kwa vilabu kadhaa - ikiwa ni pamoja na Monaco - msimu wa kiangazi baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kuambiwa atakuwa chaguo la kwanza la kocha wa Manchester United Ruben Amorim msimu huu. (The i Paper - Usajili unahitajika)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: