Liverpool ina mataumaini kuwa itafanikiwa kumshawishi mlinzi wa Ufaransa Ibrahima Konate, 26, kusaini kandarasi mpya huku klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester City zikimuwania. (TBR Football)
Kiungo wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 28, analengwa na Manchester United. (Football Insider)
Klabu ya Bayern Munich inajiandaa kumpa kandarasi ya muda mrefu mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo klabu hiyo ya Ujerumani kutoka Chelsea. (Bild - kwa Kijerumani - usajili unahitajika)
#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni