Timu ya Tanzania ya kriketi jana tarehe 24 Septemba, 2025 iliibuka na ushindi wa kishindo wa wickets 6 dhidi ya timu ya taifa ya Kenya katika mchezo wao wa pili wa kirafiki kuelekea ICC Men’s T20 World Cup Africa Regional Final 2025.
Kwa upande wa kupiga, Ajith Augustin aling’ara kwa kupata nusu karne (50 mbio kwa mipira 39), akisaidiwa na Abhik Patwa aliyefunga mbio 39. Wote wawili waliongoza mashambulizi kwa uthabiti. Kwa upande wa kupiga bola, Khalidy Juma alitoa mchango mkubwa kwa kupata 3/10 na kutunukiwa Mchezaji Bora wa Mechi, huku Ally Kimote naye akipata 3/21.
Maandalizi makubwa yanaendelea nchini Harare kuelekea mashindano makubwa ya ICC Men's T20 World Cup Africa Regional Final 2025.
#Official-Isharoja✍🏾

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni