Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Mipango ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dkt. Ephraim O. Mdee tarehe 03 Oktoba, 2025 amezindua Kikao cha Kamati ya Ufuatiliaji na Tathimini ya TRA.
Uzinduzi huo ameufanya mkoani Morogoro ambapo katika hotuba yake mbele ya wajumbe wa kamati hiyo amesema kwamba, kamati hiyo itakua inapitia maandiko dhana na taarifa za tathimini mbalimbali zitakazokua zinafanyika ndani ya Mamlaka katika mwaka husika wa fedha na kutolewa ushauri kabla ya kuwasilishwa kwenye Menejimenti na bodi ya TRA
Ameongeza pia kuwa, kamati hiyo itasaidia katika kutoa ushauri wa kuboresha zaidi mfumo unaotumiwa wa Usimamizi na Tathimini (Monitoring and Evaluation Management System-MEMS) katika kutolea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Mpango wa mwaka kwa Idara za makao makuu na Mikoa ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Kamati hiyo inaongozwa Mwenyekiti Profesa, Issaya Jairo Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA). Aidha wajumbe wa Kamati hiyo ni Nahoda P Nahoda (Mkurugenzi Msaidizi Utawala) Idara ya Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala, Eunice A. Liheluka (Kamishina Msaidizi Kodi za Ndani Divisheni ya Walipa Kodi Wadogo), Agness C. Kitwanga (Mkurugenzi Msaidizi TEHAMA, Divisheni ya Miundombinu), Ephraim Kibasa (Mkurugenzi Msaidizi Ukaguzi wa Ndani), Anna Mndeme (Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Fedha), Marko Nkya (Meneja wa Usimamizi wa Mikataba Idara ya Manunuzi), Paschal B.N Mallya (Meneja wa Ufuatiliaji na Tathimini) ambaye ndiye Katibu wa kamati hii.







Hakuna maoni:
Chapisha Maoni