Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limejipanga kisawasawa kushiriki mashindano ya michezo yanayoratibiwa na Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ambapo tarehe 28 Oktoba, 2025 limezindua rasmi vifaa vilivyofadhiliwa na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi ( Adaptation fund) vitakavyotumika na wanamichezo katika mashindano hayo.
Akizungumza wakati kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semesi amesema michezo ni muhimu kwa Afya ya binadamu kwani hupelekea uwezo wa kufanya kazi vizuri huku akisisitiza usimamizi na uhifadhi wa Mazingira nchini
Ameongeza kuwa ushiriki wa NEMC katika michezo hiyo ni fursa muhimu ya kuifikia jamii, kuimarisha ushirikiano baina ya watumishi wa Umma na Sekta binafsi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Michezo - NEMC Bw. Fortinatus Patrick amesema timu za NEMC ziko tayari kwenda kupambana katika michezo yote na wamejiandaa kufanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (NEMC) Bw. Dickson Mjinja ambaye ni mlezi qa timu hiyo, alipozungumza amesema NEMC imejipanga kisawasawa kuwa washindani na si washiriki katika michezo yote iliyo jisajili.
NEMC kwa kushirikiana na Mradi wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi umefanikisha Mandalizi hayo ya SHIMMUTA 2025 yanayotarajiwa kuafanyika jijini Mwanza November 13 - 29, 2025 huku ikilenga kuelimisha umma wa watanzania kuhusu mazingira na masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni