Muigizaji maarufu wa filamu nchini Nigeria, Regina Daniels, anaripotiwa kuondoka nyumbani kwa mume wake, bilionea Ned Nwoko, kufuatia madai ya muda mrefu ya unyanyasaji wa majumbani na msongo wa kihisia.
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na blogu ya Lagos Lately, Regina alihama katika makazi yao ya kifahari baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni miaka kadhaa ya mateso ya kimwili na kihisia.
Katika video inayosambaa mitandaoni, Regina anadaiwa kusikika akisema:
“Katika nyumba ya Ned Nwoko mimi si kitu, lakini kwenye nyumba yangu mimi ni malkia. Siwezi kuvumilia tena vurugu imezidi.”
Ripoti hizo zinaeleza kwamba wakati Regina alikuwa akihamisha mali zake, mume wake alidaiwa kutuma watu kumfuata, lakini kaka yake, Sammy Daniels, aliingilia kati kumlinda. Aidha, mashahidi wamedai kuwa Regina alikiri kuwa amekuwa akijifanya kwa muda mrefu wakati akipitia ukatili huo kimyakimya.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna tamko rasmi lililotolewa na Regina Daniels au Ned Nwoko kuhusu tukio hilo.
Blogu ya Lagos Lately imekemea vikali aina zote za ukatili wa majumbani na imemshauri Regina kutafuta msaada wa kitabibu na kisheria, huku ikizitaka mamlaka husika kuchunguza suala hilo.
Madelemo News inasisitiza umuhimu wa amani katika ndoa na inapinga kwa nguvu zote aina yoyote ya ukatili wa majumbani.
🌐 Chanzo: Lagos Lately Blog
© 2025 Madelemo News – Habari




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni