Sekondari ya Sayansi Tanga Girls – Tanga (Sh. bilioni 4.1) Chini ya Rais Samia, ujenzi wa shule ya wasichana ya sayansi iliyoko Mkoa wa Tanga Tanga Girls umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.1 Shule hii ina jumla ya wanafunzi 606 (wanafunzi wa kidato cha kwanza 136, wakidato cha tano 261 na wa kidato cha sita 209). Tafiti za Benki ya Dunia zinaonyesha kuwa kila dola moja ya Marekani inapowekezwa kwenye elimu huzalisha hadi dola 16 kwenye uchumi, huku zaidi ya asilimia 70 ya utajiri wa nchi zilizoendelea unatokana na nguvu kazi yenye maarifa na tija.
Hii ndiyo sababu kuu inayomsukuma Rais Samia kuwekeza katika elimu kwa kujenga shule za sayansi kwa wasichana kwenye kila mkoa na shule za vipaji maalum kwa wavulana kwenye kila kanda.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni