Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Ndugu Mary Pius Chatanda (MCC), ametoa wito kwa wananchi wa Jimbo la Kondoa Mjini kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kupiga kura kwa amani na kuwachagua wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ngazi zote.
Chatanda alitoa wito huo leo Oktoba 26, 2025, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika Uwanja wa Sabasaba, Kondoa Mjini, ambapo amewaombea kura Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea wa Ubunge wa Jimbo hilo, Ndugu Mariam Ditopile, pamoja na Madiwani wote wa CCM.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni