Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) imetangaza marufuku ya papo hapo ya matumizi ya misafara (escort), ving’ora (sirènes) na taa za dharura (gyrophares) katika maeneo yote ya nchi. Hatua hii imekuja kama sehemu ya mkakati wa kurejesha nidhamu na utulivu katika barabara za taifa hilo.
Tangazo hilo limetolewa Jumanne, 9 Desemba 2025, na Makamu wa Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani, Jacquemain Shabani, kufuatia agizo rasmi kutoka Ikulu ya Rais.
Lengo la Marufuku Hii
Kwa mujibu wa serikali, hatua hiyo inalenga kufanya maboresho kadhaa muhimu ikiwemo:
- Kurejesha utulivu na nidhamu ya barabarani
- Kukomesha matumizi mabaya ya ving’ora na misafara inayofanywa na watu binafsi au baadhi ya maafisa
- Kulinda usalama wa wananchi
- Kupunguza ajali zinazotokana na misafara isiyo rasmi
Utekelezaji na Usimamizi
Vikosi vya usalama vimeelekezwa kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa kikamilifu bila upendeleo. Serikali imesisitiza kuwa hatua hii ni muhimu katika kuimarisha mfumo wa usafiri na kuongeza usalama wa raia na watumiaji wa barabara.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni