Mamlaka ya hali ya hewa, Tanzania Meteorological Authority (TMA), imetoa angalizo la uwepo wa vipindi vifupi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba katika saa 24 zijazo.
Kwa mujibu wa utabiri huo, maeneo mengi nchini yatakuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo, huku vipindi vya jua vikijitokeza kwa muda mfupi. Aidha, mikoa ya Pwani ikijumuisha Mafia, kusini mwa Morogoro pamoja na Mtwara na Lindi inatarajiwa kuwa na mvua za hapa na pale, wakati Kanda ya Ziwa na Magharibi ikiwa na mawingu kiasi na mvua chache.Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na uwezekano wa mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni