Kwa mujibu wa Don Jazzy, alianza safari hiyo kwa kumuomba rafiki yake amtumie akaunti za wasichana wenye vipaji vya kuimba. Bila kuchelewa, akapewa jina la Ayra Starr anayejulikana pia kama “Sabi Girl.” Alipoingia kwenye ukurasa wake, hakusita kubonyeza “follow,” akivutiwa na vibe na uwepo wake wa kipekee mtandaoni. Ilikuwa kama bahati kukutana na kipaji kilichokuwa kinasubiri mtu sahihi kukiangazia.
Kinachofuata kinaweza kusemwa ni hadithi ya filamu siku moja Ayra Starr aliposti video akiimba, Don Jazzy akaiona na hapo ndipo mlango wa mafanikio ulipofunguka rasmi. Kutoka Instagram hadi kuwa moja ya sauti kubwa barani Afrika, safari yao inaacha somo moja muhimu: wakati mwingine, ndoto zako zinaweza kuanza kwa “post” moja tu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni