Ronaldo ameonekana akiwa na mtindo mpya wa nywele, huku sasa akielekeza nguvu zake kwenye maandalizi ya msimu mpya akiwa na Al Nassr.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 41 anaendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika soka la Saudi Arabia, na kurejea kwake mazoezini kunaongeza matarajio kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Kwa Ronaldo, lengo linaonekana kuwa moja kuendelea kufunga mabao na kusaidia Al Nassr kupigania mataji katika msimu mpya.
Mashabiki wa Al Nassr sasa wanasubiri kumuona nahodha huyo akianza tena safari yake ya kutafuta mabao na mafanikio akiwa na klabu hiyo ya Saudi Arabia.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni