Breaking


Jumanne, 11 Agosti 2026

NGAO YA JAMII 2026: STEVE BARKER AWEKA BAYANA LENGO LA SIMBA DHIDI YA YANGA

Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema timu yake imejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans SC (Yanga), utakaochezwa kesho, Agosti 12, 2026.

Barker amesema Simba inalenga kuanza msimu wa 2026/27 kwa mafanikio kwa kushinda taji hilo, huku akisisitiza kuwa maandalizi ya timu yamejikita katika maeneo mbalimbali.

“Tunataka kuuanza vizuri msimu mpya wa 2026/27 kwa kuchukua Ngao ya Jamii,” amesema Barker.

Kocha huyo amesema wanaingia kwenye mchezo huo wakitambua ubora wa Yanga, hivyo wamefanya maandalizi ya kutosha katika upande wa kiufundi, kimwili, kiakili na kisaikolojia.

Amesema wachezaji wanaelewa umuhimu wa mchezo huo na wanatambua matarajio yaliyopo kwa klabu na mashabiki wake.

Barker ameongeza kuwa Simba ni timu inayolenga kushinda katika kila mashindano inayoshiriki, akiamini maandalizi waliyofanya yatawasaidia kupata matokeo mazuri dhidi ya Yanga.

“Simba ni timu ya mataji na kesho tunaingia kwa lengo la kushinda taji,” amesema Barker, akieleza dhamira ya timu hiyo kuelekea mchezo huo.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii unatarajiwa kuwa sehemu ya maandalizi ya timu hizo kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huku Simba na Yanga zikiwa miongoni mwa timu zinazotajwa kuwa na ushindani mkubwa katika soka la Tanzania.


Hakuna maoni: