Breaking


Jumamosi, 26 Julai 2025

SINGIDA YANG’AA KWA REGGAE! RASTAFARIAN WAMSHEREKEA MFALME HAILE SELASSIE KWA MBWEMBWE


 Mtaa wa Sabasaba, kata ya Mpunguzi jijini Dodoma, uligeuka kuwa kisima cha muziki, mshikamano, na amani baada ya mamia ya waumini wa imani ya Rastafari kutoka kona mbalimbali za Tanzania na mataifa ya nje kuungana kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.

Katika hali ya furaha na utulivu, mitetemo ya nyimbo za reggae zenye ujumbe wa haki, uhuru na mshikamano zilitawala hewa, huku washiriki wakiimba, kucheza na kusali kwa heshima ya kiongozi huyo wa kihistoria anayeheshimiwa kama alama ya ukombozi wa Mwafrika na Baba wa imani ya Rastafari duniani.

Maadhimisho hayo yaliambatana na vipindi vya mafunzo ya kihistoria juu ya maisha ya Mfalme Selassie, aliyezaliwa tarehe 23 Julai 1892 na kutawala Ethiopia kati ya mwaka 1930 hadi 1974.

“Kwa sisi Rastafari, Selassie ni zaidi ya mfalme. Ni nembo ya utu wa Mwafrika, mshikamano na haki za binadamu. Siku yake ya kuzaliwa ni siku takatifu ya kutafakari na kusherehekea hadhi ya Mwafrika duniani,” alisema mmoja wa washiriki kutoka Arusha.

Mbali na kumkumbuka Mfalme Selassie, waumini hao pia walimtaja Mwalimu Julius Nyerere kama kiongozi shujaa aliyesimama na kutetea Umoja wa Afrika, akifananishwa na Selassie kwa maono na ujasiri.

Maadhimisho haya yameacha alama kubwa ya mshikamano, wakituma ujumbe wa amani, upendo na umoja—si tu kwa Rastafarian, bali kwa kila Mwafrika anayeamini katika utu, haki na heshima ya asili yake.

#MadelemoNews #RastafariTanzania #HaileSelassieDay #ReggaeForUnity #SingidaVibes

Hakuna maoni: