Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limemtambua mwanafunzi wa Darasa la Sita, **Jackline Eliabi** wa Shule ya Msingi Manyinga, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, kwa uwasilishaji wake bora wa dhana ya Uchumi Mzunguko katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Jackline alipata pongezi na kutunukiwa zawadi baada ya kuwasilisha kwa umahiri dhana hiyo muhimu inayohamasisha matumizi endelevu ya rasilimali, upunguzaji wa taka na uhifadhi wa mazingira. Uwasilishaji wake ulionesha uelewa mkubwa wa masuala ya mazingira na mchango wa wanafunzi katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kwa maendeleo endelevu.
Zawadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, ikiwa ni kutambua mchango wa wanafunzi katika kusukuma gurudumu la uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini. Dkt. Semesi alieleza kuwa wanafunzi ni wadau muhimu katika juhudi za kulinda mazingira na kwamba wao ndio mabalozi wa baadaye wa mazingira watakaosaidia kuendeleza agenda ya maendeleo endelevu kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni