Real Madrid wako tayari kutoa pauni milioni 100 kwa kiungo wa Manchester City na Hispania Rodri, 29 (Sun).
Winga wa Manchester City na England Jack Grealish, 29, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wa upande wa kushoto wanaofuatiliwa na Napoli (Corriere dello Sport).
Javi Guerra amekataa ofa ya kurefusha mkataba wake na Valencia, huku Manchester United ikiripotiwa kumfuatilia kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 22 (Marca).
Tottenham wanamfuatilia kwa karibu Kobbie Mainoo, huku kiungo huyo wa Manchester United bado hajafikia makubaliano ya kurefusha mkataba wake wa muda mrefu, ambao unamalizika mwaka 2027 (tbrfootball.com).
West Ham watashindana na Everton katika mbio za kumsajili Douglas Luiz kutoka Juventus baada ya Aston Villa kujiondoa kwenye mbio za kumsajili tena kiungo huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 (Sun).

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni