Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Petro Magoti amesisitiza kufanya kazi kwa bidii hasa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ili iweze kuleta tija ikiwa ni kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kukuza maendeleo.
Magoti ameyasema hayo akiwa katika ziara ya Katibu Tawala Mkoa wa Pwani ,Pili Mnyema katika kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.
Aidha amesema kuanzia jumamosi atarudi Wilayani hapo ili kuangalia maendeleo ya miradi inayokamilishwa na kufuatilia utekelezaji wa maelekezo yalitolewa na Katibu Tawala.
Akiwa wilayani Mafia Katibu Tawala mkoa, amekagua mradi wa ujenzi wa soko la Kilindoni unaogharimu zaidi ya Milioni 700, Ujenzi wa Jengo la wazazi kakika Hospitali ya Wilaya unaogharimu zaidi ya milioni 500 pamoja na Maboresho ya majengo ya Shule ya Msingi Utende yanayogharimu zaidi ya sh. Milioni 100.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni