Breaking

Ijumaa, 15 Agosti 2025

MAMELODI SUNDOWNS WAMPA THANK YOU NEO MAEMA MASHABIKI WA SIMBA WAFURAHIA

 

Kiungo mshambuliaji Neo Maema ameagwa rasmi na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka minne yenye mafanikio makubwa.


Mamelodi Sundowns wamemuaga Maema hii leo kwa sherehe ndogo za kuonyesha shukrani kwa mchango wake kwenye klabu, zikijumuisha michezo mikubwa na mataji aliyoisaidia timu kushinda. 

Mashabiki na wachezaji wenzake walimpa heshima na maneno ya pongezi kwa vipaji na uadilifu wake uwanjani.


Hii habari imeleta furaha kwa mashabiki wa Simba SC nchini Tanzania, Neo Maema anahusishwa kujiunga na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 

Kuja kwake Simba kunatarajiwa kuongeza nguvu ya kati na mshambuliaji, huku mashabiki wakitarajia kushuhudia ushirikiano wa kipekee wa Maema na wachezaji wengine wa timu hiyo.


Maema, ambaye amekuwa kiungo muhimu kwa Mamelodi Sundowns, atakumbukwa kwa michango yake mikubwa, hasa katika mechi za mataji ya ligi na mashindano ya kimataifa. 

Mashabiki wa Simba wanamsubiri kwa shauku ili awe sehemu ya kikosi chao katika msimu ujao.


Hakuna maoni: