RASMI: Klabu ya Simba imethibitisha kunasa saini ya kiungo mshambuliaji raia wa Afrika Kusini 🇿🇦 Neo Maema kutoka Mamelodi Sundowns kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine mmoja.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mzoefu kwenye michuano ya Afrika anatua msimbazi baada ya kudumu kwa miaka nne (4) Mamelodi Sundowns.
Tayari kiungo huyo ameungana na wachezaji wenzake kwenye kambi ya Simba sc huko nchini Misri akiungana na kocha Fadlu Davis ambaye pia ni raia wa Afrika Kusini sambasamba na beki Rushine De Reuck ambaye pia ametua Simba sc akitokea Mamelodi Sundowns.
Usajili wa Neo Maema unakuwa usajili wa tisa (9) mpaka sasa kwa wekundu wa msimbazi Simba sc baada ya usajili wa beki Rushine De Reuck, Kiungo Alassane Maodo Kante, Winga Morice Abraham, Kiungo Mkabaji Hussein Daudi Semfuko kutokea klabu ya Coastal Union, Jonathan Sowah kutokea Singida Black Stars, winga Mohamed Bajaber kutokea Kenya Polisi ya nchini Kenya, mlinzi wa kushoto Anthony Mligo kutokea klabu ya Namungo Fc na beki kiraka Naby Camara.
#Anoldmathias255 ✍🏽

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni