Breaking


Alhamisi, 7 Agosti 2025

SHAMBULIO LA MOYO HUATHIRI WANAWAKE ZAIDI KULIKO WANAUME-SWAMY


Magonjwa ya shambulio la Moyo huathiri zaidi wanawake kuliko wanaume, huku ikielezwa kuwa idadi kubwa ya Watanzania wanakimbilia zaidi India kutibiwa magonjwa ya Mifupa. 

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya ndani ya mwili, Narendra Swamy, kutoka Hospitali ya Ramaiah ya India wakati akizungumza na viongozi wa Chama Cha Waandishi Wanawake Tanzania-TAMWA.

Dokta Swamy ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ramaiah Hospital ya India amesema sababu za magonjwa ya shambulio la moyo kuathiri zaidi wanawake kuliko wanaume ni wanawake kutokufanya mazoezi na vichocheo alivyo navyo mwanamke. 

Akifafanua kuhusu ugonjwa wa saratani, Dokta Swamy amesema hakuna sababu maalum iliyothibitishwa kuwa ndicho chanzo cha saratani duniani.

Hata hivyo, amesema, kuna njia za kuzuia uwezekano wa kupata saratani na kusema, kufanya mazoezi ikiwemo ya kutembea kwa angalau dakika 30 kwa siku. 

‘Tutashirikiana kutoa mafunzo kwa wanachama wa TAMWA, madaktari wetu watatoa mada kadhaa zinazowahusu wanawake ikiwamo ukomo wa hedhi, balehe na magonjwa mengine yasiyoambukiza,” amesema Dokta Swamy

Naye, Mkurugenzi wa TAMWA, Dokta Rose Reuben ameishukuru Hospitali ya Ramaiah kwa ushirikiano ambao imekuwa ikitoa katika shirika lao ikiwemo elimu ya magonjwa ambayo yanawasumbua wanawake wa umri tofauti. 

Mitindo ya maisha ya watu waishio mjini mara nyingi unawakwamisha kufanya mazoezi na kula chakula chenye virutubisho vya kutosha kwa wakati, hali inayosababisha ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza kama shambulio la moyo.

Hakuna maoni: