Breaking


Jumapili, 3 Agosti 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA : NEWCASTLE WAMSAKA BENJAMIN SESKO, LIVERPOOL YAIMARISHA DAU LA KUMSAJILI ISAK

 

Newcastle United wamewasilisha dau la pauni milioni 65.5 kumnunua mshambuliaji wa Slovenia na RB Leipzig Benjamin Sesko, 23. (Sky Sports), wa nje.

Lakini Leipzig wanataka kipengele cha mauzo kiongezwe kwenye mkataba huo kabla ya kufikiria kukubali ofa ya Sesko. (Telegraph - Subscription Required)

Manchester United bado iko kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili Sesko, ambaye bado hajaamua kati ya Manchester United au Newcastle. (Fabrizio Romano)

Liverpool itawasilisha ombi la pili kwa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, ikiwa Newcastle watapata mbadala wake. (Daily Mail)

Arsenal walifikiria kumnunua Isak kabla ya kumsajili mchezaji mwenzake Viktor Gyokeres lakini walikuwa na mashaka juu ya rekodi ya utimamu wa afya yake (ESPN).

Hakuna maoni: