Mchezaji wa Karate Ramadhani Khamis Nassoro amechaguliwa kuiwakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya dunia ambayo yatafanyika nchini Hungary mwezi wa 11 mwaka huu.
Mchezaji huyo amechaguliwa na kamati ya ufundi ya shirikisho la karate Tanzania (TSKF) baada ya mafunzo kwa wachezaji na waamuzi wa mchezo wa Karate nchini Tanzania yaliyomalizika Septemba 20, 2025 katika klabu ya upanga jijini Dar es salaam.
Tayari Tanzania imepata mualiko kushiriki katika mashindano hayo ya dunia.
#Official-Isharoja✍🏾

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni