Breaking

Ijumaa, 19 Septemba 2025

NDUGU ZANGU SUMU HAIONJWI TUSIFANYE MAKOSA-MTATURU.

MBUNGE mstaafu wa Jimbo la Ikungi Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),Miraji Mtaturu,amewaomba wana Ikungi Magharibi kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu wa Octoba 29,2025,bali wamchagua mgombea urais kupitia chama hicho Rais Samia Suluhu Hassan,mgombea ubunge Elibariki Kingu na madiwani wanaotokana na CCM.

Mtaturu ametoa ombi hilo katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Ikungi Magharibi,ikiwa ni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

"Niwaombe ndugu zangu tuipe kura CCM,niwakumbushe tu sumu siku zote haionjwi,tusifanye makosa ya kuchagua viongozi kutoka vyama vingine,"amesema.

Hakuna maoni: