Breaking

Ijumaa, 19 Septemba 2025

DRAMA MPYA KWA STEFON DIGGS: MTOTO NJE YA NDOA AWASHA MOTO KATI YAKE NA CARDI B!

 

Wiki haijaisha vizuri kwa staa wa Buffalo Bills, Stefon Diggs. Baada tu ya yeye na Cardi B kuthibitisha wanatarajia mtoto wao, amejikuta akivutwa kwenye drama nyingine ya mahakamani kuhusu uhalali wa mtoto! 😳👶


👉 Mwanamitindo maarufu Aileen Lopera (anayejulikana pia kama Lord Gisselle) anadai Diggs ndiye baba wa binti yake Charliee Harper Diggs-Lopera, aliyezaliwa Aprili 2025. Kupitia wakili wake, Lopera anataka Diggs atambuliwe rasmi kama baba na pia achangie gharama zote—kutoka ujauzito, kujifungua hadi ada za mawakili.


⚖️ Kwa upande wake, Diggs hajakubali madai hayo moja kwa moja na ameomba kipimo cha DNA kuthibitisha ukweli. Taarifa zinaonyesha kuwa tayari mahakama iliagiza kipimo hicho kifanyike Julai 2025, lakini majibu bado hayajatolewa.


💥 Endapo itathibitishwa kweli yeye ni baba, Diggs amesema atasimama kidete kuhakikisha anashiriki kikamilifu kwenye malezi na mahitaji yote ya mtoto huyo.


Sasa mashabiki wamebaki kushangaa: Je, drama hii ya kifamilia itaathiri vipi maisha yake ya kimapenzi na Cardi B? 😮🔥


Hakuna maoni: