Tarehe 10 Februali 2026 ilkuwa ni siku ya majonzi kwa familia ya mzee Hamis Biteko sababu ilikuwa ni siku ya kuupumzisha mwili wa Marehemu Majaliwa HAMIS Biteko kwenye makazi yake ya milele.
siku hiyo ya jumanne ilikuwa siku ya majonzi kwa Mhe Doto Mashaka Biteko ambaye ni baba mdogo wa Marehemu Majariwa.
CHANZO CHA MAUTI YAKE
Majaliwa Hamis Biteko mwenye umri wa miaka (20) alifariki baada ya kupata ajari ya gari jumamosi ya Febrari 7 2026 barabara ya mjini Musoma mkoani Mara,baada ya siku mbili akazikwa innallilah wannlilah rajou.
Mwili wa marehemu Majaliwa ulipumzishwa kijijini kwao BUlangwa na kuudhuliwa wa viongozi mbalimbali wa chama na Serikali,mkuu wa mkoa wa Geita mhe Martine Shigella aliongoza maelfu ya watu kwenye mazishi hayo,mbunge wa jimbo la Hai mhe Sashisha Mafuwe naye alikuwepo,katibu wa CWT,Misalaba pia alikuwepo,Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Geita bila kusahau Kamati ya Siasa na ilishiriki mazishi hayo ya mpendwa wetu Majaliwa.
Majaliwa umeondoka wakati wana Geita wanakuhitaji,jamii inakuhitaj,umetuachia majonzi,kweli kazi ya Mungu haina makosa ila kwa miaka (20) duniani tulianza kupata ujuzi wako,
tutakukumbuka sana kwenye ^JUNIOR NDANI YA BUKOMBE^,marehemu Majaliwa alikuwa ana kipaji cha pekee ila dah!,kifo hiki.
Kweli wanadamu tuna mda mfupi duniani angalia Marehemu Majaliwa kaishi kwa miaka (20) tu,Majaliwa kalala Mwanahabari mwenzetu ndio harudi tena kwa kheri Majaliwa tutaonana Paradiso.
Marehemu Majaliwa alikuwa ni mwenye maono, Majaliwa huhuyu alipenda kujifunza,kufundisha na kushirikisha jamii maarifa aliyoyapata,dah Majaliwa umetuacha sisi,mbona mapema.
Hakika marehemu Majaliwa Hamis Biteko ameacha pengo kubwa sana katika familia,tasnia ya uandishi wa habari,sekta ya Madini na moyo ya walaji (WASOMAJI) wake wengi



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni