Breaking

Jumamosi, 20 Septemba 2025

NEMC NA DEPO WAFANYA SHUGHULI YA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA USAFI DUNIANI


 Katika kuadhimisha Siku ya Usafi Duniani hii leo, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Miradi ya Mazingira Dar es Salaam (Depo), wamefanya shughuli ya usafi katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam.

Zoezi hili limehusisha watumishi wa hospitali, wananchi pamoja na wadau wa mazingira, ambapo maeneo mbalimbali ya hospitali yamesafishwa kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio hilo, Meneja wa NEMC kanda ya Mashariki Kaskazini, Glory Kombe, amesema kuwa usafi wa mazingira ni msingi wa afya bora, huku akihimiza jamii kushiriki kikamilifu katika kampeni za kitaifa za usafi wa mazingira.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Depo, Humphrey Milinga, amesema ni muhimu kwa sekta binafsi na taasisi za serikali kutoa elimu zaidi kuhusu usafi wa mazingira, ili kulinda afya za wananchi na kuhakikisha mazingira yanabaki safi.













Kampeni hii imeongeza hamasa kwa jamii ya Mwananyamala kushiriki kikamilifu katika jitihada za kulinda mazingira, na pia ni kielelezo cha mshikamano wa kitaifa katika kujenga Tanzania yenye afya na ustawi wa mazingira.

Hakuna maoni: