Breaking

Jumamosi, 20 Septemba 2025

NMB YADHAMIRIA KUSAIDIA MAENDELEO YA RELI NA UCHUMI WA NCHI

 

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna,amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Shiwa, jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamelenga kujadili maeneo ya ushirikiano kati ya Benki ya NMB na TRC, hususan katika kuunga mkono juhudi za kitaifa za kukuza maendeleo ya miundombinu na kuimarisha uchumi wa taifa.


Kwa ushirikiano huu, Benki ya NMB inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimkakati ili kuchochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi nchini.


#NMBKaribuYako

Hakuna maoni: