Benki ya NMB imeshiriki kikamilifu katika Mkutano wa 18 wa Wakaguzi wa Ndani uliohusisha taasisi mbalimbali za umma na binafsi, uliofanyika jijini Arusha. Ushiriki huu unaonyesha dhamira ya NMB katika kukuza utawala bora na kuimarisha mifumo thabiti ya udhibiti wa hatari.
Kupitia jitihada endelevu katika kuzingatia misingi ya utawala bora, NMB imeendelea kupata heshima kubwa kimataifa. Benki imetambuliwa kama Benki Bora Zaidi nchini katika masuala ya Kijamii, Mazingira na Utawala Bora (Best ESG Bank) pamoja na Benki Salama Zaidi Tanzania (Safest Bank in Tanzania).
Ujumbe wa NMB katika mkutano huo uliongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Benedicto Baragomwa, akifuatana na Meneja wa Tawi la Clock Tower, Praygod Mphuru, pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Kwa NMB, ushiriki huu ni ushahidi wa kuendelea kuwekeza katika mifumo ya uwajibikaji, uwazi na utawala bora kwa maendeleo endelevu ya sekta ya fedha nchini.
#SafestBank #NMBKaribuYako



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni