Breaking

Jumatano, 10 Septemba 2025

SUMU HAIONJWI TENA MCHAGUENI MASSABURI - JAKAYA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete amezindua kampeni katika jimbo la kivule, na kuwaombea kura wagombea wa CCM.

Akiwanadi na kuwakabidhi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025 /30 Ojambi Masaburi mgombea Ubunge jimbo la kivule,  na wagombea  wa  udiwani  6  kata ,  Mwenyekiti mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete  amewaambia wananchi wasijaribu uongozi kwa vyama vingine. 

Amesema Chama Cha Mapinduzi, kimewasimamisha wagombea wazuri akiwepo Dokta Samia Suluhu Hassan nafasi ya Urais,  Ojambi Masaburi na madiwani wenye uwezo mkubwa na wanatosha kuwa viongozi.

Akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo hilo Ojambi Masaburi, Jakaya amesema ni kijana mwenye uzoefu, na hajifunzi uongozi  hivyo apewe kura ili aendeleze kazi na miradi ya maendeleo. 

Kikwete, amesema katika jimbo la Kivule miradi ya maendeleo kwenye sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu na uchumi imeendelea kuwekewa fedha na Rais Samia Suluhu Hassan hivyo kukichagua Chama Cha Mapinduzi ni kuchagua maendeleo. 

Katika Mkutano huo, Jakaya amebainisha mafanikio makubwa 

yamepatika katika awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, upande wa diplomasia ya kimataifa. 

Amebainisha kuwa Rais Samia, amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliko kipindi chochote kwenye uongozi wake jambo linaloipa sifa Tanzania upande wa kimataifa. 

Uzinduzi wa kampeni hizo ni mwendelezo wa kampeni katika majimbo ya Mkoa wa Dar es salaam, uliosimamisha wagombea ubunge na madiwani.

Hakuna maoni: