Breaking

Jumanne, 23 Septemba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE: LIVERPOOL NA BARCELONA ZAMGOMBANIA ALVAREZ

 

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Julian Alvarez, 25, anafikiria kuondoka Atletico Madrid msimu ujao, huku Liverpool na Barcelona zikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina. (Fichajes - kwa Kihispania)

Wasiwasi wa West Ham kuhusu mahitaji ya kifedha ya Nuno Espirito Santo unaweza kutoa mwanya kwa Slaven Bilic kuchukua nafasi ya Graham Potter, ambaye anang'ang'ania kibarua chake baada ya mwanzo mbaya wa The Hammers msimu huu. (Guardian)

Barcelona inataka kufikia makubaliano na Manchester United ili kumsajili mshambuliaji wa Uingereza ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkopo Marcus Rashford, 27, kwa £26m - ada ambayo haikidhi kiwango kinachotakiwa na United, ya takribani na £35m. (Star)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: