Breaking

Jumanne, 30 Septemba 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE: TOTTENHAM, MAN UNITED, MANCHESTER CITY NA ASTON VILLA ZAMWANIA SEMENYO

 

Mshambulizi wa Bournemouth Antoine Semenyo anaendelea kuvutia nia licha ya kusaini kandarasi mpya msimu wa joto, huku Tottenham, Manchester United, Manchester City na Aston Villa zikimhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (TBRFootball)

Arsenal wako kwenye mazungumzo na winga Bukayo Saka, 24, kuhusu kandarasi mpya ambayo itamfanya kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo. (Express External,)

Newcastle wanataka kumpa beki wa zamani wa Uingereza Kieran Trippier mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Chronicle, external)


#ChanzoBbcswahili

Hakuna maoni: