Breaking

Ijumaa, 26 Septemba 2025

WAJASILIAMALI MKOANI KIGOMA WAASWA KUJIUNGA NA KUCHANGIA NSSF

Wajasiriamali mkoani Kigoma wamehimizwa kujiunga na kuchangia katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, NSSF, kwa lengo la kujihakikishia ulinzi wa kijamii, kupambana na majanga ya kiuchumi na maandalizi ya maisha ya uzeeni. Wito huo umetolewa leo, Septemba 25, na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mheshimiwa Balozi Simon Sirro, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NSSF STAA WA MCHEZO, PAKA RANGI awamu ya pili, inayolenga kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo kwa njia ya ubunifu unaogusa maisha yao ya kila siku. Ambayo iliyoambatana na zoezi la ugawaji wa majiko ya gesi kwa Mama na Baba Lishe ambao pia ni wanachama wa NSSF pamoja na baadhi ya wastaafu.  

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, ameeleza kuwa Mfuko umepewa dhamana ya kuhakikisha kila Mtanzania ikiwemo waliojiajiri wanapata huduma bora za hifadhi ya jamii, kinga dhidi ya majanga ya kiuchumi pamoja na mafao mbalimbali. Mbali na hilo, aliongeza kuwa NSSF imetoa majiko ya gesi kwa Mama na Baba Lishe kama sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, ili kuboresha mazingira yao ya kazi na kulinda afya. Huku Meneja wa Usimamizi wa Mafao wa NSSF, Bw. James Oigo, akitoa ufafanuzi juu ya viwango vya uchangiaji kwa wanachama waliojiajiri kupitia Mpango wa Hifadhi Skimu, ambapo amesema kuwa mfumo huo ni rafiki na unazingatia uwezo wa kipato wa wananchi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.









Kwa ujumla, kampeni hii inaendelea kuwa chachu ya mabadiliko kwa wajasiriamali nchini, ikilenga kujenga jamii yenye uelewa wa kutosha kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii nchini.

Hakuna maoni: