Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
(i) Bw. Fortunatus Makore Magambo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Kabla ya Uteuzi huu, Bw. Magambo alikuwa Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi katika Mfuko huo; na
(її)
Bw. Plasduce Mkeli Mbossa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni