Breaking

Jumanne, 16 Desemba 2025

UFANISI WA BANDARI ZA TPA WAONGEZEKA, BANDARI YA DAR ES SALAAM YAONGOZA KWA ASILIMIA 36

 

Ufanisi wa uhudumiaji wa shehena mbalimbali katika Bandari za TPA umeongezeka, huku bandari ya Dar es Salaam  ufanisi wake ukizidi kuimarika na  shehena kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 36 kwa mwaka, kasi ambayo haijapata kutokea tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa 18 wa Tathimini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi uliofanyika katika kituo  cha  mikutano  cha kimataifa Arusha (AICC) Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile amesema, ufanisi unaoshuhudiwa kulingana na takwimu za shehena zaidi ya Milioni 34,000,000 zinazohudumiwa katika Bandari zote nchini za mwambao wa Bahari na Maziwa Makuu ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Amesema mpango wa mradi mkubwa wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao na Bagamoyo unaoendea sambamba na maboresho ya bandari za maziwa, matumizi ya vifaa vya kisasa na mifumo ya kisasa ya TEHAMA,  imesaidia kuongezeka kwa shehena inayoingia na kutoka kupitia katika bandari zote nchini.


Katika salamu zake za ukaribisho Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema, kasi ya ukuaji wa Bandari si ya kawaida kwani imekuwa ikiongezeka kwa asilimia 36 kwa mwaka.


Aidha amesema ushindani ni muhimu kwa sababu unaleta changamoto ya kufanya vizuri zaidi  na kuwekeza zaidi katika Bandari zetu.




Sambamba na mkutano huo wa tathimini,Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi zinashiriki kwenye maonyesho  yanayoambatana na mkutano yanayofanyika  katika viwanja vya AICC.

Hakuna maoni: