Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Asharose Migiro amewasili na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa chama ngazi ya mkoa wa Arusha, viongozi wa dini pamoja na maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid kwaajili ya kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ambaye mda mchache baadaye atanadi Ilani ya CCM (2025/30) ,Sera na Ahadi zake pamoja na kuomba kura.
Dkt. Migiro amefika na kunyoosha kamba ya uelekeo wa Oktoba 29 ambapo amewahamasisha na kutoa wito kwao kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa kumchagua Dkt. Samia, Wabunge na Madiwani wa CCM.
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais ndani ya mkoa wa Arusha leo tarehe 2 Oktoba 2025.
#SafariYaCCM
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#OktobaTunatiki🇹🇿✅






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni