Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 10 Oktoba 2025, akiwa katika Kata ya Kabungu, Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi, kwenye Mkutano wa Kampeni, ameinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akieleza mafanikio makubwa yaliyofanyika Chini ya uongozi madhubuti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Pamoja na mambo mengine Chatanda kupitia Mkutano huo wa Kampeni, alimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanganyika, Moshi Selemani Kakoso, pamoja na Madiwani wa Kata kwa tiketi ya CCM, kupitia Jimbo hilo.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni